Posts

Showing posts from August, 2017

KUMCHA BWANA 1

Image
Jina la BWANA lisifiwe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!  Ndugu msomaji katika page hii ashukuriwe MUNGU awezaye kutenda mambo makubwa na magumu kuliko yale tuyawazayo na tuyatendayo kwa maana njia zake na akili zake hazichunguziki wala hazitafutikani.  WARUMI 11:33-36. Ni wakati mwingine tena nakualika katika somo jingine tena katika kuendelea kutafakari ukuu na uumbaji wa MUNGU katikati ya ulimwengu huu, somo ambalo ninakuletea leo hii ni somo lenye kichwa kinachosema  “KUMCHA MUNGU NDIO MWANZO WA MWANADAMU KULIFIKIA AGANO LA MUNGU” kutokana na somo hilo leo hii tutaangalia tu kwa ufupi utangulizi juu ya somo hilo. Ndugu msomaji kwa ufupi somo hili lina kuja kwaajili ya kukuonyesha tu kwa ufupi kwamba MUNGU  ameweka maagano (Ahadi)  mengi sana katika maisha ya mwanadamu sambamba na kwamba maisha ya mwanadamu ni mafupi kutokana na dhambi ambazo zinafanywa na mwanadamu huyuhuyu ambaye MUNGU amemwekea ahadi nyingi. Sasa fuatana nami katika somo hili tukitafakari ...