KUMCHA BWANA 1
Jina la BWANA lisifiwe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Ndugu msomaji katika page hii ashukuriwe MUNGU awezaye kutenda mambo makubwa na magumu kuliko yale tuyawazayo na tuyatendayo kwa maana njia zake na akili zake hazichunguziki wala hazitafutikani.
WARUMI 11:33-36. Ni wakati mwingine tena nakualika katika somo jingine tena katika kuendelea kutafakari ukuu na uumbaji wa MUNGU katikati ya ulimwengu huu, somo ambalo ninakuletea leo hii ni somo lenye kichwa kinachosema “KUMCHA MUNGU NDIO MWANZO WA MWANADAMU KULIFIKIA AGANO LA MUNGU” kutokana na somo hilo leo hii tutaangalia tu kwa ufupi utangulizi juu ya somo hilo.
Ndugu msomaji kwa ufupi somo hili lina kuja kwaajili ya kukuonyesha tu kwa ufupi kwamba MUNGU ameweka maagano (Ahadi) mengi sana katika maisha ya mwanadamu sambamba na kwamba maisha ya mwanadamu ni mafupi kutokana na dhambi ambazo zinafanywa na mwanadamu huyuhuyu ambaye MUNGU amemwekea ahadi nyingi. Sasa fuatana nami katika somo hili tukitafakari somo hili kutoka katika ZABURI 25:12-14 “Ni nani amchaye BWANA? Atamfundisha katka njia anayoichagua. Nafsi yake itakaa hali ya kuifanikiwa; Wazao wake watairithi nchi. Siri ya BWANA iko kwao wamchao, naye atawajulisha agano lake”. Katika mstari huo wa 25 biblia inaonesha kwamba MUNGU anatuuliza swali kupitia kinywa cha mwimba Zaburi kuwa anataka kumjua mtu anayemcha YEYE yaani anayemtegemea BWANA maana yake inawezekana ameona ya kwamba katika maisha yetu, imani zetu, makusanyiko yetu n.k tuna kutana lakini si kwa viwango vya kumcha yeye, hivyo anakuja kwa kinywa cha mwimba Zaburi kwamba “ni nani amchaye BWANA?” na kutoa jibu la swali hilo kwa kusema “atamfundisha katika njia anayoichagua………………………………………….” .
Maana yake ni kwamba sambamba na maagano yaani Baraka/Ahadi ambazo mungu ameziweka kwaajili ya mwanadamu lakini ili mwanadamu aweze kufikia ahadi hizo huambatana na nguvu ya kuchagua iliyopo ndani mwake. MWANZO 30:19-20 “Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, Baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; kumpenda BWANA, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi BWANA aliyo waapia baba zako, Ibrahim, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa”.
Kwahiyo huu ndio mfumo ambao MUNGU aliweka ndani ya mwanadamu kwaajili ya kupima viwango vya mwanadamu vya kumcha yeye , sasa ili MUNGU ajue kwamba mtu umekaa vizuri mbele zake anaangalia ni jinsi gani mwanadamu ameweza kuitumia kwa usahihi ile nguvu ya kuchagua iliyopo ndani mwake. Sasa baada ya kuangalia hayo yote pamoja na kwamba MUNGU aliweka nguvu ya kuchagua kwa mwanadamu bado ikawa si kipimo tosha cha kumpima mwanadamu mwenye viwango vya kumcha MUNGU, kama ni hivyo basi tuangalie sifa nyingine au vigezo vinavyo angaliwa na MUNGU juu ya mtu anayemcha yeye,
1. Moyo wako kuishi kwa kuitafakari njia ya BWANA. MITHALI 16:9 “Moyo wa mtu huifikiri njia yake; bali BWANA huziongoza hatua zake” Hii ni moja ya sifa ambayo MUNGU huiangalia kwa mtu mwenye viwango vya kumcha yeye, MUNGU ananena kwetu kupitia kinywa cha mtumishi wake Sulemani kwamba anatambua kuwa ndani ya mwanadamu kuna udhaifu ndiyo maana anasema moyo wa mtu huifikiri njia yake, lakini kwa kulijua hilo MUNGU akasema huziongoza hatua zake. Maana yake hata kama moyo wa mwanadamu ni mdhaifu kiasi gani lazima mwanadamu utafute uongozi wa MUNGU ndani yake kama msaada pale ambapo moyo unakuwa umezidiwa na dunia ili kukurudisha katika njia ya unyoofu yaani njia ya BWANA. Lakini pia BWANA kuongoza hatua zako hutokea tu pale ambapo mwanadamu anapotambua ya kwamba amebeba kusudi la MUNGU ndani yake na kutengeneza mazingira ya kuongozwa na yeye ndipo BWANA anapotupa roho mtakatifu kama msaidizi wetu katika kutuongoza kuijua kweli yake, Rejea zaburi 25:12.
2. Kujitenga na uovu. AYUBU 28:28 “Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, na kujitenga na uovu ndio ufahamu”. Ndugu msomaji, moja ya vitu ambavyo pia MUNGU hupima viwango vya mwanadamu vya kumcha yeye ni namna mtu anavyoweza kujitenga na uovu. Soma HOSEA 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa;mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya MUNGU wako, mimi nami nitawasahau watoto wako”.Biblia inasema “kwa kuwa umeyakataa maarifa, mimi nami nitakusahau wewe….” Kumbe kuyapokea maarifa ya MUNGU ni mwanzo wa mwanadamu kuwa karibu na MUNGU. Je! Maarifa nini? Maarifa ni dira ambayo inamwongoza mtu katika maisha yake ili kuweza kuchagua lililojema na lililobaya. Sasa basi bibilia inaposema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa maana yake mtu mwenye maarifa tayari anauwezo wa kuchagua kwa usahihi yaani kutenganisha jambo baya na jema ndiyo maana biblia ikasema kwa kuwa umeyakataa maarifa mimi nami nitakukataa wewe hii inamaana kuwa mtu aliye kataa maarifa ameikataa kweli ya MUNGU na kuambatana na uovu na sio kujitenga na uovu. Kwa hiyo ili mwanadamu aweze kujitenga na uovu ni lazima awe amekubali kupokea maarifa ya MUNGU. Jiulize kwanini wasomi wengi ndio wanaomaliza pombe katika majumba ya starehe au kwanini wasomi wengi wanatumia sigara ilihali sigara hizohizo zimeandikwa ni hatari kwa afya yako, jibu ni kwamba wasomi wengi wanaelimu lakini sio maarifa. Chanzo cha maarifa ni kimoja tu ambacho ni kumcha BWANA na si vinginevyo SOMA MITHALI 1:7A.
3. Kuishi kwa kutenda mema. 2TIMOTHEO 3:17 “ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema”. Mungu katika maisha yetu huangalia mwanadamu anaishi kwa kutenda mema mangapi, hivyo Mungu hupima viwango vyetu kwa kuangalia uwezo wetu wa kutenda mambo mema maana huo ndio ukamilifu wa mwanadamu. Biblia inaposema mtu wa Mungu maana yake kila mwanadamu aliyepo chini ya jua ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu lakini huyu mwanadamu hawezi kuonekana amekamilika mbele za Mungu kama bado hana uwezo wa kutenda mema ndio maana biblia ikamaliza kwa kusema “amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema”. Hivyo ishi kwa kutenda yaliyo mema ili Mungu akuone ya kwamba umekamilika.
4. Unyenyekevu katika kuomba na kuwa mtu wa toba. 2NYAKATI 7:14 “ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu,watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia kutoka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao”. Mungu anatukumbusha habari ya unyenyekevu yaani kukubali hali ya kwamba sisi ni wanadamu ambao tayari tuna dhambi lakini sambamba na hayo yote lazima tukubali ya kwamba Mungu ndiye aliye mkuu kuliko kitu chochote na mmiliki wa mbingu na nchi hivyo hata katika kuomba kwetu Mungu hupima viwango vyetu ni kwa jinsi gani tunaweza kujishusha mbele zake. Lakini pia kitu kikubwa ambacho Mungu huangalia pia ni Roho ya kuomba toba pale ambapo kama wanadamu tunakosa mbele zake, wakati Fulani tunaweza pita hata katika magumu kwa kuto kuwa wepesi wa kukubali kosa ndio maana katika mstari huo biblia inasema “na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia kutoka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao”. Mpendwa katika vitu ambavyo Mungu anavichukia ni pale anapoona mwanadamu ametenda dhambi na kuendelea kuishi katika hiyo dhambi lakini pale ambapo tutachukua uamuzi wa toba yeye atatusamehe na kuiponya nchi yetu, na kama sisi tutakuwa tumekwisha kusamehewa basi tayari tumetengeneza mazingira ya kuurithi ufalme wake pia.

Comments
Post a Comment