KIJANA NA USAFI WA MAISHA YA KIKRISTO
KIJANA
NA USAFI WA MAISHA YA KIKRISTO.
UTANGULIZI:
Nakukaribisha msomaji katika tafakari ya
somo jingine linalohusu kijana na maisha ya kikristo ni jinsi gani kijana aishi
maisha Matakatifu kama inavyompendeza Mungu na si kuwafurahisha tu wanadamu
katika maisha yetu tukimchukiza MUNGU.
Kristo ni mpakwa mafuta. Ambaye ni tofauti
na watu wengine. Sasa basi Ukiwa kama kijana wa kikristo ambaye umebatizwa kwa
Roho Mtakatifu ndani mwako na si tu kwa ishara ya Wanadamu ya nje tambua kuwa
Mungu amekuweka kwa kusudi lake kama mpakwa mafuta umzalie matunda kwa njia ya
Kristo YESU.
WARUMI 7:4 “Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa
njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika
wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda”.
Hivyo basi ili kijana wa Kijana wa
kikristo awe katika viwango vya usafi wa maisha ya kiroho lazima kufuata na
kutafakari neno hili.
1THESALONIKE 4:1-8
"Iliyobaki, ndugu, tunakusihini na
kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi
iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo
mpate kuzidi sana. Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu.
Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;
kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika
hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu. Mtu asimpunje ndugu yake
wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha
haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana. Maana Mungu
hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso. Basi yeye anayekataa, hakatai
mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu".
i.
Kijana wa Kikristo lazima aweke mipaka
ya ukuaji wake.
Ukisoma katika mstari wa kwanza unaonesha
kuwa Mkristo ni lazima aenende katika Bwana Yesu maana yake lazima kuwe na
mpaka/utofauti kati ya kijana wa Kikristo na kijana asiye wa Kikristo. Si
kwamba kama kijana asiyemwamini Yesu Kristo anakuwa Mlevi, Mzinzi, Mwasherati,
Mwizi, Mwongo n.k. lakini na wewe kijana wa kikristo ukaonekana unayafanya haya
bado utaonekana ndani mwako hakuna kweli ya Kristo.
ii.
Kusudi la Mungu kijana wa Kikristo
atakaswe.
1THESALONIKE 4:3
“Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa
kwenu, mwepukane na uasherati;”
Uasherati ni kufanya
tendo la ngono kwa mtu au kijana ambaye hajaoa au kuolewa ambayo ni tofauti pia
na uzinzi ambao mtu anafanya tendo la ngono akiwa ameolewa au kuoa na mtu
ambaye siye mke au mme wake. My dear vijana wengi shetani ametushikilia kwenye
suala hili la uasherati maana miili yetu inawaka kwa kuukimbilia uasherati hata
tukashindwa kuweka usafi wa mwili na ROHO zetu na kumkosea MUNGU wetu.
iii.
Kijana wa Kikristo ni lazima ajue
kuutunza mwili wake.
1THESALONIKE 4:4
“kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake
katika utakatifu na heshima;”
Vijana wa Kikristo ni wale wanaoweza kuimudu
miili yao ambapo inakuwa inawaka tamaa ya uasherati hivyo ndivyo Biblia
inavyosema kwamba kuuweza mwili yaani kuhakikisha unaweza kuongoza mwili na sio
mwili kukuongoza. Lakini hili pia haliwezekani kama kijana wa kikristo
hajatambua thamani ya mwili wake. Jiulize kama kijana wa kikristo mwili wako
una thamani gani? Maana kuna vijana wamethaminisha miili yao na chipsi, soda,
nguo, pombe n.k. lakini jua ya kwamba hakuna kitu cha thamani kuufikia mwili
wako zaidi ya damu ya Yesu Kristo.
iv.
Mungu anataka Vijana wa Kikristo
tusiharibiwe katika suala la mahusiano.
1THESALONIKE 4:7-8
“Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe
katika utakaso. Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa
ninyi Roho wake Mtakatifu".
Mungu anamtaka kijana
wa Kikristo kuishi maisha ya kuendelea kuwa mtakatifu na kuto kumkosea Mungu
ndio maana katika kitabu cha warumi anasema tumeitwa ili tumzalioe Mungu matunda
na ukisoma katika aya hii ya saba inasema hatujaitiwa uchafu bali tuishi katika
hali ya utakatifu yaani utakaso. Mungu alijua kabisa kwamba mwanadamu peke yake
hawezi kuishi katika hali hiyo ya utakaso ndio maana akaweka amri kumi. Lengo
la amri zake Mungu ni kutulinda na kutupa mahitaji tunayoyahitaji kwa wakati
sahihi.
NB. MOYO SAFI KWA MWANZO MPYA.
v Pamoja
na kufanya Dhambi au maovu mengi lakini MUNGU anaweza kukusamehe na kukufanya
mpya
NOTE. MAISHA MAPYA YA KIKRISTO.
v Maisha
mapya ya mahusiano ya kikristo ni kumpenda Kristo kwanza. DANIELI 1:8.
Still alive
ReplyDelete