WAJIBU WA KIONGOZI (P3)
WAJIBU
WA KIONGOZI KIBIBLIA (P3)
Ndugu msomaji katika
somo lililopita sehemu ya kwanza na ya pili tuliangalia wajibu wa kiongozi
kibiblia, na jinsi gani kiongozi wa KIMUNGU awe, vitu anavyoweza kufanya na
asivyoweza kufanya kama hukubahatika kusoma sehemu ya kwanza bofya “http://injilikamiliyayesu.blogspot.com/2017/08/jina-la-bwana-lisifiwe-ndugu-msomaji.html”
na
kama hukusoma sehemu ya pili bofya “http://injilikamiliyayesu.blogspot.com/2017/09/wajibu-wa-kiongozi-p2.html”
Lakini katika mwendelezo wa somo hili
leo nataka tuangalie kitu kingine juu ya kiongozi kibiblia ambacho kinakuhusu
wewe na mimi kama viongozi ambao tumepewa mamlaka ya kuvitiisha viumbe vyote
chini ya jua. MWANZO 1:26-27
Somo hilo ni “MAZINGIRA YA KIONGOZI WA KIROHO/KIMUNGU”.
Kutokana na somo hili Mungu ametupa kibali
cha kumiliki kila aina ya kiumbe kilichopo duniani yaani hata wanadamu wenzetu.
Maana yake jinsi ulivyo ni kiongozi yaweza kuwa katika familia, katika jamii,
katika ukoo au namna nyingine yoyote wewe ni kiongozi. Ila tambua kuwa katika
kuongoza kwako haijalishi utapitia yepi? Jua Mungu amekuweka ili usipoteze hata
kimoja katika mamlaka aliyokupa.
YOHANA 18:4-9
“Basi Yesu, hali akijua yote yatakayompata, akatokea, akawaambia, Ni nani mnayemtafuta? Wao wakamjibu, Ni Yesu Mnazareti. Yesu akawaambia, Ni mimi. Yuda naye aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao. Basi alipowaambia, Ni mimi, walirudi nyuma, wakaanguka chini. Basi akawauliza tena, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti. Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao. Ili litimizwe lile neno alilolisema, Wale ulionipa sikumpoteza hata mmoja wao”.
Katika mazingira hayo tunaona Yesu jinsi
alivyo kubali hata kuingia katika mateso ili tu asipoteze kile alichokabidhiwa
na Mungu mwenyewe. Swalik je! Kile ambacho Mungu alikukabidhi bado unacho?
Maana wengi tumepoteza hata utu wetu kwa kuitamani dunia ikiwemo tama ya pesa
leo hii huna thamani tena je! Kama umepoteza thamani yako tu vitu ulivyo kabidhiwa
vitakuwa salama? Jibu ni hapana.
Lakini hebu tusome KUTOKA 3.1 “Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu”. Sasa kupitia kifungu hicho tujifunze mazingira ambayo kiongozi wetu wa mfanoMUSA alipitia sambamba na kwamba aliamza kwa safari ya kuongoza kundi la YETHRO na baadae hadi Mungu akampandisha thamani kwenda kuongoza wana wa Israeli.
Mambo ya kujifunza ni haya yafuatayo:-
i.
Kuwavusha watu na kufika nyuma ya mlima
yaani kuto wapitisha watu katika mazingira magumu kwa njia ya kumshirikisha
Mungu.
Jangwa
ni matatizo katika kuongoza, vikwazo katika kuongoza au mazingira magumu katika
uongozi.
ii.
Kama kiongozi unahitaji kuwa mfano au
kielelezo kwa wengine (role model).
Kwa
mfano, kuna vitu wewe unavyo wengine hawana
Kuna vitu ambavyo wengine
wanavifanya wewe hupaswi kuvifanya.
Kuna vitu ambavyo wengine
wanashabikia wewe hupaswi kushabikia.
Kuna vitu vizuri vya Kimungu ambavyo
unatakiwa uvifanye ili wenginewatamani kuiga kutoka kwako.
1TIMOTHEO 4:11-13
“Mambo hayo uyaagize na kuyafundisha. Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi. Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma na kuonya na kufundisha”.
Biblia inatukumbusha kuwa tufanye bidii
katika kufundisha na sisi wenyewe kuwa kielelezo katika mambo haya yafuatayo:-
Usemi
Maana yake maneno ambayo unaongea na watu na
ubora uliobeba uongozi wa Roho Mtakatifu.
Mwenendo
Tabia na Matendo lazima yawe kama kiongozi wa
Kimungu
Usafi
Kiongozi lazima awe msafi wa kimwili na Roho
kuanzia mavazi yake, mwili wake mpaka usafi wa Roho yake binafsi. MUNGU
ATUSAIDIE.
NB: MUSA pamoja na kwamba YETHRO mkwewe alimwona kama mtu wa kuchunga kundi la wanyama wake hadi nyuma ya mlima mtakatifu wa Mungu, lakini Mungu bado alimwona kuwa yeye ni kiongozi wa kuwatoa wana wa Israeli mikononi mwa mateso ya Farao. KUTOKA 3:1-10.
Usiangalie wanadamu wana
kuonaje lakini mwangalie Mungu anakuonaje HATA WEWE NI KIONGOZI!!!!!!!!!!!
TEMBELEA page yangu ya
FACEBOOK “Injili Kamili Ya YESU” Whatsup namba +255658443473 na private call
+255766966930
.............................MWISHO.........................
Comments
Post a Comment