WAJIBU WA KIONGOZI {P2}
WAJIBU WA KIONGOZI
KIBIBLIA {P2}.
2
TIMOTHEO 2:14-16
“Uwakumbushe mambo
hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana
faida, bali huwaharibu wasikiao. Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na
Mungu, mtenda kazi asiyekuwa na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno
la kweli. Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa
wataendelea zaidi katika maovu,”
Katika mistari hiyo tunajifunza wajibu wa
kiongizi kama ifuatavyo:-
i. Kiongozi lazima awe hodari. Yaani kuwa
jasiri katika kuwakumbusha watu kweli ya Mungu “ukiwaonya machoni pa Mungu”
katika kuonya wewe kama kiongozi unahitaji kuondoa Roho ya hofu, mashaka na wasiwasi
katika kutoa ushauri ulio sahihi.
ii. Kama kiongozi ni lazima usimamie kweli
na maadili kwa uhodari mkuu. Ukiwa kama kiongozi umepewa neon la Mungu kama
katiba au dira katika kufanya maamuzi hivyo katika kusimia kweli ya Mungu
lazima uwe na msimamo wa neno linasema nini na si watu unaowaongoza wanahitaji
nini japo kuna wakati hitaji hilo lina umuhimu katika kundi lakini je! Kipi ni
kusudio kuu kwa wakati huo. “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu,
mtenda kazi asiyekuwa na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la
kweli.”
iii. iii.
Kiongozi ndiye mtu wa kuangalia uongozi
mpya. Maana yake kiongozi yeyote lazima awe na “FUTURE VISION” kwaajili ya nani
anaweza kushika fimbo yake kwaajili ya kuliongoza kundi maana yake kiongozi
lazima atengeze mfumo wa uongozi kama Mungu alivyotengeneza mfumo wa viongozi
katika kuongoza wana wa Israeli, yaani
MUSA----JOSHUA----YUDA>>>>>. Maana yake anachukua jukumu la
kuangalia kiongozi mwenye sifa njema, mwenye uhodari, mwenye uaminifu na mwenye
kufanya kazi kwa bidii.
iv.
iv. Kiongozi awe na ushuhuda na mwakilishi
mzuri na mshauri mzuri kwa kila jambo baya ambalo linatokea katika eneo lake la
kazi.
v.
v. Kiongozi lazima awe kielelezo kwa wale
anao waongoza katika sehemu yake ya kazi 2TIMOTHEO 4:1-5.
vi.
vi. Kiongozi anatakiwa kutojihusisha na
migogoro inayo endelea katika eneo lake la kazi kwa mfano migomo. Hiyo
huonyesha ya kwamba yeye amekubaliwa na Mungu ili atumike sawasawa na kusudi la
Mungu.
vii. vii.
Kiongozi anatakiwa kubebeana mizigo na
viongozi wenzake na pia kubeba mizigo ya kundi analoliongoza maana yeye ndiye
mwakilishi wa kundi.
viii. vii.
Kujiepusha na maneno ambayo hayana
maadili yaani yasiyo ya dini au yasiyo ya kiMungu kwa mfano matusi na lugha
nyingine chafu.
NB: MUSA pamoja na
kwamba YETHRO mkwewe alimwona kama mtu wa kuchunga kundi la wanyama wake hadi
nyuma ya mlima mtakatifu wa Mungu, lakini Mungu bado alimwona kuwa yeye ni
kiongozi wa kuwatoa wana wa Israeli mikononi mwa mateso ya Farao. KUTOKA
3:1-10.
Usiangalie wanadamu
wana kuonaje lakini mwangalie Mungu anakuonaje HATA WEWE NI KIONGOZI!!!!!!!!!!!
Comments
Post a Comment