WAJIBU WA KIONGOZI {P1}
WAJIBU WA KIONGOZI
KIBIBLIA {P1}.
2Timotheo
1:8-9
“Basi usiuonee haya
ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie
mabaya pamoja nami kwaajili ya injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu; ambaye
alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi,
bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika
Kristo Yesu tangu milele,”
Jambo ambalo tunalipata hapo juu ya wajibu
wa kiongozi ni:-
i.
Kiongozi ni lazima awe na ushuhuda
kwaajili ya Kristo yaani kushuhudia katika uongozi wake ni wangapi wangapi
wamempokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao yaani kuachana na njia za
uasi wa kale na kukubali kuwa hapo mwanzo waliishi katika hali ya dhambi na
sasa kupitia wewe kama kiongozi wameachana na uasi wao na kumgeukia Mungu kwa
kuamini kuwa yeye ndiye kiongozi wao.
ii.
Kiongozi ni lazima ajue kwamba ameitwa
kutumika na sio kutumia. Ndio maana biblia katika mstari huo wa 8 inasema “bali
uvumilie mabaya pamoja nami kwaajili ya injili” lakini biblia haikuishia hapo,
katika mstari wa 9 inasema “alituokoa akatuita kwa mwito Mtakatifu, si kwa
kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye….” maana
yake kwamba tumeitwa kuwa viongozi kwaajili ya kutimiza kusudi la Mungu
mwenyewe si kwaajili ya kutimiza mahitaji yetu pekee. Hivyo kama Mungu ametuita
kwa kusudi lake lazima tutumike sawa na kusudi lake si kutumia tu vile vitu ambavyo
Mungu ametupa au watu ambao ametupa kwaajili ya kuwaongoza.
NB: MUSA pamoja na
kwamba YETHRO mkwewe alimwona kama mtu wa kuchunga kundi la wanyama wake hadi
nyuma ya mlima mtakatifu wa Mungu, lakini Mungu bado alimwona kuwa yeye ni
kiongozi wa kuwatoa wana wa Israeli mikononi mwa mateso ya Farao. KUTOKA
3:1-10.
Usiangalie wanadamu wana
kuonaje lakini mwangalie Mungu anakuonaje HATA WEWE NI KIONGOZI!!!!!!!!!!!!!
Comments
Post a Comment