KUMCHA BWANA 2



Jina la BWANA lisifiwe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Ndugu msomaji katika page hii ashukuriwe MUNGU awezaye kutenda mambo makubwa na magumu kuliko yale tuyawazayo na tuyatendayo kwa maana njia zake na akili zake hazichunguziki wala hazitafutikani. WARUMI 11:33-36.
Ni wakati mwingine tena nakualika katika somo jingine tena katika kuendelea kutafakari ukuu na uumbaji wa MUNGU katikati ya ulimwengu huu, somo ambalo ninakuletea leo hii ni somo lenye kichwa kinachosema  “KUMCHA MUNGU NDIO MWANZO WA MWANADAMU KULIFIKIA AGANO LA MUNGU” kutokana na somo hilo leo hii tutaangalia tu kwa ufupi utangulizi juu ya somo hilo.
Ndugu msomaji kwa ufupi somo hili lina kuja kwaajili ya kukuonyesha tu kwa ufupi kwamba MUNGU  ameweka maagano (Ahadi)  mengi sana katika maisha ya mwanadamu sambamba na kwamba maisha ya mwanadamu ni mafupi kutokana na dhambi ambazo zinafanywa na mwanadamu huyuhuyu ambaye MUNGU amemwekea ahadi nyingi. Sasa fuatana nami katika somo hili tukitafakari somo hili kutoka katika ZABURI 25:12-14 Ni nani amchaye BWANA? Atamfundisha katka njia anayoichagua. Nafsi yake itakaa hali ya kuifanikiwa; Wazao wake watairithi nchi. Siri ya BWANA iko kwao wamchao, naye atawajulisha agano lake”.
Katika mstari huo wa 25 biblia inaonesha kwamba MUNGU anatuuliza swali kupitia kinywa cha mwimba Zaburi  kuwa anataka kumjua mtu anayemcha  YEYE yaani anayemtegemea BWANA maana yake inawezekana ameona ya kwamba katika maisha yetu, imani zetu, makusanyiko yetu n.k tuna kutana lakini si kwa viwango vya kumcha yeye, hivyo anakuja kwa kinywa cha mwimba  Zaburi kwamba “ni nani amchaye BWANA?”  na kutoa jibu la swali hilo kwa kusema “atamfundisha katika njia anayoichagua………………………………………….”

Maana yake ni kwamba sambamba na maagano yaani Baraka/Ahadi ambazo mungu ameziweka kwaajili ya mwanadamu lakini ili mwanadamu aweze kufikia ahadi hizo huambatana na nguvu ya kuchagua iliyopo ndani mwake. MWANZO 30:19-20 “Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, Baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; kumpenda BWANA, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi BWANA aliyo waapia baba zako, Ibrahim, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa”.

  Kwahiyo huu ndio mfumo ambao MUNGU aliweka ndani ya mwanadamu kwaajili ya kupima viwango vya mwanadamu vya kumcha yeye , sasa ili MUNGU ajue kwamba mtu umekaa vizuri  mbele zake anaangalia ni jinsi gani mwanadamu ameweza kuitumia kwa usahihi ile nguvu ya kuchagua iliyopo ndani mwake.




Comments

Popular posts from this blog

NGUVU ILIYOPO KATIKA NENO LA MUNGU

KIJANA NA USAFI WA MAISHA YA KIKRISTO

WAJIBU WA KIONGOZI {P2}