Posts

Showing posts from 2018

MAOMBI YA KUOMBEA IMANI.

Image
MAOMBI YA KUOMBEA IMANI:   UTANGULIZI.     Ndugu msomaji nakukaribisha katika hili ili likusaidie kukuza viwango vyako vya kiimani na kusimama vizuri katika wokovu wako. Kuombea imani ni jambo ambalo kwa mwamini yeyote haliwezi kukwepeka maana mtaji wa wokovu na utakatifu ni IMANI hivyo pasipo imani hakuna utakatifu na wokovu.      Mara nyingi watu wana kuwa na mikesha, ibada za maombi n.k lakini katika kuomba kwetu wengi huwa tunasahau kuombea kitu kimoja ambacho ni imani zetu. Imani zetu kama wakristo zinatakiwa kuombewa maana imani zipo katika viwango vinavyopimika yaani kiwango kidogo cha IMANI na kiwango kikubwa cha imani. Ili imani iweze kuwa katika kiwango kikubwa ni lazima iombewe na sababu ya kiwango cha imani kuwa chini ni kuto kuombea imani hiyo. Lakini katika hayo yote lazima tutambuwe kuwa imani inayotakiwa ni ile ambayo ipo katika kiwango kikubwa {cha juu}. Swali:- kwanini tuombee imani? LUKA 22:31-34   “Akasems, Simo...