MAOMBI YA KUOMBEA IMANI.
MAOMBI YA KUOMBEA IMANI:
UTANGULIZI.
Ndugu msomaji nakukaribisha katika hili ili likusaidie kukuza viwango vyako vya kiimani na kusimama vizuri katika wokovu wako. Kuombea imani ni jambo ambalo kwa mwamini yeyote haliwezi kukwepeka maana mtaji wa wokovu na utakatifu ni IMANI hivyo pasipo imani hakuna utakatifu na wokovu.
Mara nyingi watu wana kuwa na mikesha, ibada za maombi n.k lakini katika kuomba kwetu wengi huwa tunasahau kuombea kitu kimoja ambacho ni imani zetu. Imani zetu kama wakristo zinatakiwa kuombewa maana imani zipo katika viwango vinavyopimika yaani kiwango kidogo cha IMANI na kiwango kikubwa cha imani. Ili imani iweze kuwa katika kiwango kikubwa ni lazima iombewe na sababu ya kiwango cha imani kuwa chini ni kuto kuombea imani hiyo. Lakini katika hayo yote lazima tutambuwe kuwa imani inayotakiwa ni ile ambayo ipo katika kiwango kikubwa {cha juu}.
Swali:- kwanini tuombee imani? LUKA 22:31-34
“Akasems, Simoni, Simoni, tazama, shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano. Lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako. Akamwambia, Bwana, niwapo pamoja nawe, mimi ni tayari kwenda gerezani au hata kifoni. Akasema, Nakuambia, Petro, jogoo hatawika leo, kabla wewe hujanikana mara tatu ya kuwa hinijui.”
Hapo tunaona jinsi Yesu alivyokuwa akimthibitishia Petro kuwa IMANI pasipo kuombewa inatindika yaani inapungua. Hivyo lazima ujue kuwa imani inapokuwa inaombewa inampa mtu uwezo wa kukaa karibu zaidi na Mungu na kukaa mbali kabisa na dhambi ya kumkana Yesu maana mtu yeyote anayetenda dhambi ni ishara ya kumkana Yesu maana yake ndani yake hakuna hofu ya Mungu yaani imani ndio maana hata Yesu aliomsisitiza sana Petro kuwa alikuwa anamuombea ndio maana imani yake ikaonekana imesimama jambo ambalo Petro alikuwa halitambui kuwa anaonekana amesimama katika imani kwasababu Yesu ametenga muda kuiombea imani yake.
Jambo jingine ambalo mimi na wewe tunapaswa kulijua katika kuombea imani zetu ni kuwa tunaziombea zetu kwasababu jaribu lipo maana majaribu ni mtaji wa kuongoza imani lakini imani hiyohiyo inayo kuwa kutokana na majaribu isipoombea jaribu linakuwa ni shemu ya kupoteza mtaji wa imani na sio kukuza mtaji wa imani. Sasa ebu kwa ufupi tuangalie aina ya majaribu yanayotufanya tuiombee imani ili tupitapo katika hayo imani yetu iweze kuongezeka na sio kupungua.
Jaribu la 1. Majaribu ya Mungu mwenyewe. MWANZO 22:1-3
“Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, mimi hapa. Akasema umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka,ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmoja wapo nitakaokuambia. Ibrahimu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwaajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu.”
Hilo ni jaribu aina ya kwanza ambalo ndilo linalotufanya tuombee imani zetu ili tunapopita katika majaribu kama hayo yanayotoka kwa Mungu mwenyewe tusianguke bali tusimame katika kuyashinda na sio kuyakemea maana wengi wetu tunashindwa kutofautisha kati ya jaribu la Kimungu na jaribu la kishetani na ndipo inapofika wakati kila jaribu linalotujia tunaanza kulikemea baada ya kulipokea na kumwita Mungu atuonyeshe namna ya kutoka katika jaribu hilo.
Ingawa katika kitabu cha YAKOBO 1:13 inasema mtu ajaribiwapo asiseme ninajaribiwa na Mungu maana Mungu hamjaribu mtu…….. Lakini swali ni je! mbona Ibrahimu alijaribiwa na Mungu huyuhuyu? Jibu ni kwamba majaribu yanayotoka kwa Mungu ni yale anayoyatoa Mungu mwenyewe kwenda kwa mtu wake ampendaye. Ndio maana Mungu aliachilia jaribu hilo kwa Ibrahimu kwasababu alikuwa anampenda nz hata baada ya Ibrahimu kulishinda jaribu lile ndipo malaika akamwambia “sasa nimejua yakuwa unamcha Mungu……” MWANZO 22:12 kwahiyo jaribu hilo kwa Ibrahimu ulikuwa ni mtihani wa Mungu ili kumpandisha kutoka kiwango kimoja cha imani kwenda kiwango kingine cha imani. Kumbuka safari ya Ibrahimu na Mungu ilianzia toka MWANZO 12 hadi kufikia sura ya 22 Mungu alikuwa hajatambua kuwa Ibrahimu anaviwango vya kumcha Mungu hadi pale alipo kubali kulipokea jaribu lililotoka mikononi mwa Mungu.
NB: hivyo usijaribu kulikemea jaribu litokalo katika mkono wa Mungu maana ndio mtihani wako wa kukuvusha katika viwango vingine vya kiimani maana hata mwanafunzi ili aweze kupanda darasa lazima afaulu mtihani wa wa darasa analoliacha.
Jaribu la 2. Jaribu la mjaribu {shetani}. MATHAYO 4:2-4
“Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa. Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe mwana wa Mungu , amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Naye akajibu akasema, mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.”
Hapo tunaona jinsi shetani anavyo mjaribu Yesu katika patano lake na Mungu maana yake mwanadamu anaweza kuwa ameweka patano na Mungu wake lakini shetani anaingilia kati ili kuvuruga ule mpango wa Mungu. Kwahiyo mtu wa mungu usipojua namna ya kutofautisha aina hii ya majaribu na kujua namnma ya kuiombea imani iweze kutambua aina ya majaribu hutoweza kuvuka katika majaribu unayopitia na kuanguka katika majaribu ni ishara ya imani kupungua.
Jaribu la 3. Jaribu la tamaa zetu wenyewe. YAKOBO 1:14-15
“Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewehuku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile dhambi ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti”
Jaribu la tatu linalotufanya ili tuombee imani ni jaribu linalokuja kutokana na tamaa zetu jaribu hili ;limefanya kazi ya kuangusha imani za wengi kutokana na imani kuto kuombewa wengi wameanguka katika tamaa ya uzinzi, kuiba, kushuhudia uongo n.k. Lakini sababu kubwa ya haya yote ni kutokana na imani kuto kutengamaa vizuri kwa maombi na katika kitabu hicho cha Yakobo anasema na dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. Maana yake kutokana na dhambi wengi waeufikia umauti kutokana na kukosa hofu ya Mungu ambayo hupatikana tu kwa imani iliyosimama yaani imani inayoombewa.
Swali! Je! majaribu ni nini?
Kutokana na aina za majaribu tulizo zionz hapo juu JARIBU ni jambo linalomsafirisha Mkristo na kufika hadi njia panda yaani uzima na mauti. Yaani kwa Mkristo aliye simama vizuri kiimani si kila changamoto inayokuja kwako katika maisha ni jaribu bali ni kile kitu ambacho kijna kufikisha mahali ambapo unafikiri kufanya uamuzi wa kuachana na Mungu au kuendelea na Mungu hilo ndilo jaribu.
Kwa hiyo mpendwa lazima utambue kuwa msingi mkubwa wa kuombea imani ni kukusaidia kuvuka katyika majaribu na sio kuyakataa majaribu maana katika jaribu ndipo penye Baraka kwa Mkristo na siri ya kuyashinda majaribu ni kuiombea imani ili isitindike wakati wa taabu. Na imani ikiombewa maana yake unavikwa ujasiri wa kuishinda dbambi na kuwa thabiti mbele ya imani iliyo katika Kristo Yesu.
Tembelea www.injilikamiliyayesu.blogspot.com au Facebook page Injili Kamili YA YESU

MUNGU awabariki kwa mafundisho mazuri mnayotoa
ReplyDeleteAmen Amen barikiwa pia
DeleteBe blessed mtumishi
ReplyDeleteAmen
Delete