Posts

HEKIMA YA MUNGU KATIKA KUTUSAIDIA KUSIMAMA KIIMANI AU KURUDI NYUMA KIIMANI. SEHEMU YA II

Image
KIPINDI CHA PILI  II. JINSI MUNGU ALIVYOWEKA MGAWANYO  WA HEKIMA YAKE NDANI YA WATU. Kutoka 31:3-11 “nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina, ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba, na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote. Tena, tazama, nimemchagua, awe pamoja naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani; nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kufanya vyote nilivyokuagiza; yaani, hema ya kukutania na sanduku la ushuhuda, na kiti cha rehema kilicho juu yake, na vyombo vyote vya Hema; na meza, na vyombo vyake, na kinara cha taa safi pamoja na vyombo vyake vyote, na madhabahu ya kufukizia uvumba; na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote, na birika na tako lake; na mavazi yenye kufumwa kwa uzuri, na mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika katika k...

HEKIMA YA MUNGU.

Image
 SOMO: “HEKIMA  YA MUNGU KATIKA KUTUSAIDIA KUSIMAMA KIIMANI AU KURUDI NYUMA KIIMANI.” KIPINDI CHA I UTANGULIZI: MSINGI: Yakobo  3:13-18 "N'nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima. Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli. Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani. Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya. Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki. Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani." LENGO:    Kumwezesha Mkristo kuwa na maisha yenye matokeo yatokanayo na hekima iliyo ndani yake kuitafuta na kuitumia hekima hiyo katika kukabiliana na  changamoto katika maisha yake.” DONDOO ZA MSINGI: Hekima ndio/...

MAOMBI YA KUOMBEA IMANI.

Image
MAOMBI YA KUOMBEA IMANI:   UTANGULIZI.     Ndugu msomaji nakukaribisha katika hili ili likusaidie kukuza viwango vyako vya kiimani na kusimama vizuri katika wokovu wako. Kuombea imani ni jambo ambalo kwa mwamini yeyote haliwezi kukwepeka maana mtaji wa wokovu na utakatifu ni IMANI hivyo pasipo imani hakuna utakatifu na wokovu.      Mara nyingi watu wana kuwa na mikesha, ibada za maombi n.k lakini katika kuomba kwetu wengi huwa tunasahau kuombea kitu kimoja ambacho ni imani zetu. Imani zetu kama wakristo zinatakiwa kuombewa maana imani zipo katika viwango vinavyopimika yaani kiwango kidogo cha IMANI na kiwango kikubwa cha imani. Ili imani iweze kuwa katika kiwango kikubwa ni lazima iombewe na sababu ya kiwango cha imani kuwa chini ni kuto kuombea imani hiyo. Lakini katika hayo yote lazima tutambuwe kuwa imani inayotakiwa ni ile ambayo ipo katika kiwango kikubwa {cha juu}. Swali:- kwanini tuombee imani? LUKA 22:31-34   “Akasems, Simo...

NGUVU ILIYOPO KATIKA NENO LA MUNGU

Image
NGUVU ILIYOPO KATIKA NENO LA MUNGU    Karibu ndugu msomaji katika mfululizo wa masomo haya ya kibiblia kwa kutembelea www.injilikamiliyayesu.blogspot.com au facebook page “Injili Kamili YA YESU” ili kujifunza masomo mengi zaid ya Kimungu. Nakukaribisha katika somo hili jipya kwaajili ya kujifunza machache haya ambayo Mungu amenipa kibali kuyaachilia kwako kupitia kichwa cha somo kinachosema “ NGUVU ILIYOPO KATIKA NENO LA MUNGU ”.  Tuanze na kutafakari maana Kamili ya neno kibiblia.     Neno ni ujumbe wa Mungu ambao unaotumika na mwanadamu kwaajili ya kumfundisha na kumwongoza mwanadamu kuishi maisha matakatifu ya kumtafuta Mungu. Sambamba na kwamba neno la Mungu limehifadhiwa na mwanadamu kwa njia ya mandishi lakini kutokana na kukua kwa teknolojia hadi kwa njia ya sauti hili neno limehifadhiwa pia.     S asa basi neno hili ndilo ambalo Mungu ametupa kama sehemu ya msingi au njia ya mwanadamu kutatua matatizo yake kwa k...