HEKIMA YA MUNGU.


 SOMO: “HEKIMA  YA MUNGU KATIKA KUTUSAIDIA KUSIMAMA KIIMANI AU KURUDI NYUMA KIIMANI.”

KIPINDI CHA I

UTANGULIZI:

MSINGI: Yakobo  3:13-18

"N'nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima. Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli. Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani. Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya. Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki. Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani."

LENGO:

   Kumwezesha Mkristo kuwa na maisha yenye matokeo yatokanayo na hekima iliyo ndani yake kuitafuta na kuitumia hekima hiyo katika kukabiliana na  changamoto katika maisha yake.”

DONDOO ZA MSINGI:

Hekima ndio/ndicho kitu  kinachoweza kumsaidia mtu kufanya maamuzi mazuri au mabaya anapopita kwenye changamoto Fulani.

 Hivyo kama inaweza kumsaidia katika kufanya maamuzi mazuri au mabaya ni lazima Mkristo aitafute ili imsaidie.

Hivyo akiisha kuitafuta ni lazima aitumie ili kukabiliana na changamoto za maisha yake ya kila siku.

Swali:

Je! Aipataje na kuitumikiaje?

JIBU:HEKIMA hutafutwa kwa njia ya kusoma, kufundishwa na  kusikiliza neno la Mungu ilibaada ya hayo yote Mkristo aweze kufanya maamuzi sahihi yenye hofu  ya Mungu ndani yake katika changamoto anayokuwa amekutana nayo.

Hekima  ni nini?

Ni uwezo wa ndani wa kufikiri na kutenda kwa kutumia ufahamu , uzoefu na maarifa  unaoambatana na Roho ili kuleta matokeo  yaliyokusudiwa .


Hekima si kitu kinachoshikika  bali ni kitu ambacho kipo ndani ya mtu ambacho huonekana kwa jinsi mtu anavyoweza kuamua anapokutana na changamoto fulani katika maisha ya kila siku.

ROHO-Hiki ni chanzo kisichoonekana na pia nacho kimegawanyika katika makundi mawili yaani

  • Roho wa Mungu
  • roho ya shetani/dunia/roho ya kibinadamu.
  • Roho wa Mungu. Ni roho ya kiutu itokayo kwa Mungu  mwenyeweambaye ni muumba wa mbingu na nchi au tungewa kusema  hii ndiyo Roho njema.
  • roho ya shetani. Hii ni roho ya kidunia au kipepo  ambayo ndani yake imebeba aina Fulani ya uharibifu.

Mfano 1: katika maisha changamoto inaweza kuwa ni ugonjwa tena  wa aina  moja  kwa watu wawili tofauti lakini ufumbuzi wa tatizo la ugonjwa huo  huwa tofauti mmoja anaweza kutafuta tiba kwa njia ya maombi (Roho Wa Mungu) na mwingine kwa njia ya waganga wa kienyeji(roho ya shetani).

Mfano  2:  Familia moja inaweza kupatwa na msiba lakini baada ya msiba  wapo wanaoweza kwenda madhabahuni kutoa sadaka ya shukrani kwa kumaliza salama msiba (Roho wa Mungu) na wapo watakao anza kutafuta waganga wa kienyeji (roho ya shetani)  ili kujua kwa nini msiba umetokea.

Mfano  3: Nyumba mbili tofauti zinaweza kuwa na mgogoro wa ndoa unaofanana inaweza kuwa changamoto ni kukosa mtoto/watoto lakini ndoa nyingine ikavunjika kwa kukosa uvumilivu  na nyingine ikaendelea  kustawi katika kusubiri  wakati wa Bwana.

Kila kitu duniani unachokiona leo ni  matokeo ya hekima . rejea aina mbili za hekima

Ukiona kitu kizuri ujue ni matokeo ya hekima ya kiMungu

Ukiona kitu kibaya ujue ni matokeo ya hekima ya kishetani.

Mfano:

Mwizi- alienda kuiba ni matokeo ya dhiki ambayo ndani yake hekima  ya kishetani imeona suluhu  ni kuiba.

Uzinzi ;- ni  ishara ya dhiki ambayo ndani yake  hekimaya shetani  imeona  suluhu ya dhiki hiyi ni kuzini. Hata ulimwengu huu unaouona leo uliumbwa na Mungu kwa hekima yake.

Zaburi 104:24

"Ee Bwana, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. Dunia imejaa mali zako."

Hakuna jinsi ambayo mtu anaweza kua bora katika maisha kama ndani yake hakuna hekima hapa ndipo tunaangalia zaidi hekima ya Mungu ambayo ndio msingi wa somo letu .

Mambo mawili ya msingi juu ya hekima .

Uwezowa ndani.

Huu ni uwezo unaonekana katika utendaji pale unapokua na ujuzi wa jambo fulani na ujuzi huo ukiwa na nguvu ndani yake ya kuleta matokeo tarajiwa na nguvu hiyo ni Roho (Mungu/shetani). Mwanzo 41:39 “Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe.”


Roho inayoambatana na ujuzi/uwezo.

Hapa  ndipo tunaangalia aina mbili za hekima yaani hekima ya Mungu  na hekima yashetani.

Hivyo unapoona  una hekima ni muhimu sana ukaangalia ni roho ya namna gani iliyoko ndani yako. Luka 9:53-56 “Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu.Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]? Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.] Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.”


Hapo tunaona hekima ya Mungu haipo kwa ajili ya kujijenga yenyewe kwa kuwaangamiza wengine  BALI kwa kuwaokoa kutoka katika hatari .

Na ndio maana tunaona Yesu akiwakanya wanafunzi wake ambao walifikiri kutumia hekima ya dunia kwa kushusha moto ili wauteketeze mji kwa kuwa wamewakataa.

Itaendelea............!!!!!!!!!!!!!!!

BY:  Mwl. Enea Andreas Msanga

Kwa masomo mengine zaidi tembelea ukurasa wangu mtandaoni kwa tovuti ya www.injilikamiliyayesu.blogspot.com au facebook page “Injili Kamili YA YESU”

Na kwa mawasiliano zaidi piga +255(0)766966930(Whatsup) na +255(0)658443473

Comments

Popular posts from this blog

NGUVU ILIYOPO KATIKA NENO LA MUNGU

KIJANA NA USAFI WA MAISHA YA KIKRISTO

WAJIBU WA KIONGOZI {P2}