HEKIMA YA MUNGU KATIKA KUTUSAIDIA KUSIMAMA KIIMANI AU KURUDI NYUMA KIIMANI. SEHEMU YA II

KIPINDI CHA PILI  II.

JINSI MUNGU ALIVYOWEKA MGAWANYO  WA HEKIMA YAKE NDANI YA WATU.

Kutoka 31:3-11

“nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina, ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba, na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote. Tena, tazama, nimemchagua, awe pamoja naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani; nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kufanya vyote nilivyokuagiza; yaani, hema ya kukutania na sanduku la ushuhuda, na kiti cha rehema kilicho juu yake, na vyombo vyote vya Hema; na meza, na vyombo vyake, na kinara cha taa safi pamoja na vyombo vyake vyote, na madhabahu ya kufukizia uvumba; na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote, na birika na tako lake; na mavazi yenye kufumwa kwa uzuri, na mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika katika kazi ya ukuhani; na mafuta ya kutiwa, na uvumba wa manukato mazuri, kwa ajili ya mahali patakatifu; sawasawa na yote niliyokuagiza ndivyo watakavyofanya wao.” 


Mungu anapotaka kufanya matengenezo au maboresho yoyote ndani ya kanisa ni lazima kuwepo na watu waliojazwa hekima na maarifa ya kiMungu ili waweze kuifanya kazi hiyo.

Hekima na maarifa hayo ambayo Mungu hukusudia  kuweka ndani  ya watu huyaweka ili waweze kutimiza kusudi lake na kwa ajili ya utukufu wake TU.

Katika kitabu hicho cha KUTOKA  tunaona Mungu anatoa utaratibu wa kujenga madhabahu ya kufukizia uvumba na kwa kusudi hilo anaandaa watu wenye hekima  na maarifa na ufahamu ili waweze kujenga mahali hapo ambao ni BEZALELI NA  OHOLIABU ingawa maelekezo na maagizo ya ujenzi yamepita kama Musa. KUTOKA 31:1-7 “Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda; nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina, ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba, na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote. Tena, tazama, nimemchagua, awe pamoja naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani; nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kufanya vyote nilivyokuagiza; yaani, hema ya kukutania na sanduku la ushuhuda, na kiti cha rehema kilicho juu yake, na vyombo vyote vya Hema;”

MUHIMU: HIVYO ndivyo Mungu alivyoweka mpango wa kutumia hekima yake kwetu hata leo ndani  ya kanisani kwamba akitaka kufanya jambo lolote  au maboresho yoyote ndani ya kanisa  hutumia watu ili kuwapa maelekezo ya namna ya kufanya maboresho hayo au matengenezo  hayo ndani ya kanisa.

Pamoja na watu hao kupewa  maelekezo  hayo si  kila mtu anaweza  kupewa hekima  hiyo ya Mungu bali hutegemea sana uchaji wa kiMungu na bidii ya wakristo katika kumtafuta Mungu.

Hivyo ndivyo Mungu  anavyoweza kuweka mazingira ya ustawi wa kanisa kwa kutumia  watu waliobeba hekima yake kwa kusudi lake.

MHUBIRI 7:15-29 “Mambo hayo yote nimeyaona mimi katika siku za ubatili wangu, yuko mwenye haki apoteaye katika haki yake, yuko na mtu mwovu azidishaye maisha yake katika udhalimu wake. Usiwe na haki kupita kiasi; Wala usijiongezee hekima mno; Kwani kujiangamiza mwenyewe? Usiwe mwovu ku pita kiasi; Wala usiwe mpumbavu; Kwani ufe kabla ya wakati wako? Ni vizuri kwamba ulishike neno hilo; naam, hata kwa neno hilo tena usiuondoe mkono wako; kwa kuwa mtu yule amchaye Mungu atatoka katika hayo yote. Hekima ni nguvu zake mwenye hekima, Zaidi ya wakuu kumi waliomo mjini. Bila shaka hakuna  mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi. Tena, usitie moyoni mwako maneno yote yaliyosemwa; usije ukamsikia mtumwa wako mwenyewe ali anakutukana. Kwa kuwa mara nyingi moyo wako pia unajua ya kwamba wewe mwenyewe umewatukana watu wengine. Mambo hayo yote mimi nimeyahakikisha katika hekima. Nilisema, Mimi nitakuwa na hekima, lakini imefarakana nami. Mambo yale yaliyo mbali, na yale yaendayo chini sana, ni mtu yupi awezaye kuyatafuta? Nikageuka, na moyo wangu ulikazwa katika kujua na kupeleleza, na kuitafuta hekima, na maana ya mambo yaliyoko; ili nifahamu ya kuwa uovu ni upumbavu, na upumbavu ni wazimu. Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti; yaani, mwanamke ambaye moyo wake ni mitego na tanzi, na mikono yake ni kama vifungo; yeye ampendezaye Mungu atamponyoka, bali mwenye dhambi atanaswa na yeye. Tazama, asema Mhubiri, mimi nimeyaona hayo kwa kulinganisha hili na hili, ili kuitafuta jumla; ambayo bado nafsi yangu nikali nikiitafuta, nisiione; mwanamume mmoja katika elfu nimemwona; bali mwanamke mmoja miongoni mwa wote mimi sikumwona. Tazama, hili tu nimeliona; Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu, lakini wamebuni mavumbuzi mengi.”


Jambo la kujua katika  hekima ya Mungu  ni kuwa asili ya hekima ya Mungu ni Mungu mwenyewe. Na hekima hiyo ya Mungu tunaipata  kwa njia ya neno lake .

Ukisoma kitabu hicho cha mhubiri  7 mstari wa 15  anasema yupo mwenye haki anayeweza kupotea  katika haki yake na mstari wa 16 anasema  usijiongozee hekima maana yake hakuna mwanadamu anayeweza kujipa haki  yeye mwenyewe binafsi.

Lakini  pia mstari wa 18 na 19 anasema ni vyema ukalishika neno na mtu anayeshika neno ndiye atakayetoka katika uangamivu.

Swali? Kwanini mtu anayelishika neno anaweza kutoka  katika uangamivu?

Ni kutokana na hekima iliyopo ndani ya Mungu  ambayo tunaipata kupitia neno lake.

Jambo jingine tunalopaswa kulijua ni kwamba hekima ya Mungu sio mwili wa mwanadamu bali ni kipawa cha Mungu mwenyewe ambacho amekitoa kwa mwanadamu ili kutimiza kusudi lake.

Ndio maana Mungu anasema katika MHUBIRI  7:23 "Mambo hayo yote mimi nimeyahakikisha katika hekima. Nilisema, Mimi nitakuwa na hekima, lakini imefarakana nami."  SULEMANI anasema mimi nilisema nitakuwa na hekima lakini imefarakana nami. maana yake usiitetee hekima ndani yako mwenyewe bali mwombe Mungu akupe neema ya kulinda hekima iliyopo ndani yako.

 MAOMBI

Tenga muda wa kumwomba Mungu akupe uwezo wa kutumia hekima yake aliyowekeza ndani yako ili kuleta manufaa ndani kanisa.

Tenga muda wa kuombea hekima ya Mungu ndani yako ili izidi kudumu daima.

Ndani ya hekima  ya Mungu  ndipo tunapoweza kuziona hata karama za Mungu zikifanya kazi ndani ya kanisa

Hivyo kanisa pia linawajibu  wa kuomba hekima ya Mungu  ndani ya kanisa ili izae matunda.

Inawezekana leo ndani ya kanisa maendeleo hayaonekani  kwa sababu wapo watu ambao Mungu aliwekeza hekima  ndani yao lakini watu waliopewa hekima hizo wakanyamaza na hata sasa tunaona kanisa limedumaa.

MUHIMU: Kumbuka kuwa hata ujenzi wa madhabahu Mungu ameweka ufahamu na maarifa ndani ya watu hivyo ni wajibu wa kanisa kuomba juu ya jambo hili ili makanisa yaweze kukua.



Comments

Popular posts from this blog

NGUVU ILIYOPO KATIKA NENO LA MUNGU

KIJANA NA USAFI WA MAISHA YA KIKRISTO

WAJIBU WA KIONGOZI {P2}