KIJANA NA USAFI WA MAISHA YA KIKRISTO
KIJANA NA USAFI WA MAISHA YA KIKRISTO. UTANGULIZI: Nakukaribisha msomaji katika tafakari ya somo jingine linalohusu kijana na maisha ya kikristo ni jinsi gani kijana aishi maisha Matakatifu kama inavyompendeza Mungu na si kuwafurahisha tu wanadamu katika maisha yetu tukimchukiza MUNGU. Kristo ni mpakwa mafuta. Ambaye ni tofauti na watu wengine. Sasa basi Ukiwa kama kijana wa kikristo ambaye umebatizwa kwa Roho Mtakatifu ndani mwako na si tu kwa ishara ya Wanadamu ya nje tambua kuwa Mungu amekuweka kwa kusudi lake kama mpakwa mafuta umzalie matunda kwa njia ya Kristo YESU. WARUMI 7:4 “Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda”. Hivyo basi ili kijana wa Kijana wa kikristo awe katika viwango vya usafi wa maisha ya kiroho lazima kufuata na kutafakari neno hili...