DINI ILIYO SAFI NI IPI?



DINI ILIYO SAFI NI IPI?

     Karibu ndugu msomaji katika somo hili jipya ili upate kujifunza ipi ni Dini iliyosafi ambayo Mungu wetu anahitaji tumwabudu kwayo lakini kabla sijaendelea sana nikukaribishe kutembelea blog yangu kwa masomo mengi zaidi kwa kubonyeza www.injilikamiliyayesu.blogspot.com au kutembelea page ya Facebook “Injili Kamili YA YESU”. Karibuni sasa tuendelee na somo letu lenye kichwa kinachosema DINI ILIYO SAFI NI IPI? Tuanze kwa kuangalia maana halisi ya DINI.

   Dini ni utaratibu anaoutumia mwanadamu katika kumwabudu Mungu. Yaani hii tungeweza kusema ni kitu ambacho mwanadamu amekianzisha kwa akili zake kama sehemu ya kupitishia kusudi au haja zake kwa MUNGU.

   Zipo dini nyingi lakini hizi dini zote hutofautiana tu katika kitu kimoja ambacho ni “UTARATIBU/MFUMO” katika kuongoza na kumwongoza mwanadamu kuzungumza na Mungu.

   Swali: YESU kama mkombozi wa mwanadamu katika kazi ya kumkomboa mwanadamu  je! alianzisha na aliacha dini gani?

  Yesu hakuanzisha wala hakuacha dini yoyote ila aliikuta dini moja ya “KIYAHUDI” iliabudiwa na Wayahudi na ndio waliosema Asulibiwe kwa kumshudia uongo. MARKO 14:57-65Hata wengine wakasimama, wakamshuhudia uongo, wakisema, Sisi tulimsikia akisema, Mimi nitalivunja hekalu hili lililofanyika kwa mikono, na katika siku tatu nitajenga jingine lisilofanyika kwa mikono. Wala hata hivi ushuhuda wao haukupatana. Kisha Kuhani Mkuu akasimama katikati, akamwuliza Yesu, akisema, Hujibu neno? Hawa wanakushuhudia nini? Lakini akanyamaza, wala hakujibu neno. Kuhani Mkuu akamwuliza tena, akamwambia, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wake Mtukufu? Yesu akasema, Mimi ndiye, nanyi mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija na mawingu ya mbinguni. Kuhani Mkuu akararua nguo zake, akisema, Tuna haja gani tena ya mashahidi? Mmesikia kufuru yake; mwaonaje ninyi? Wote wakamhukumu kuwa imempasa kuuawa.  Wengine wakaanza kumtemea mate, wakamfunika uso, na kumpiga makonde, na kumwambia, tabiri. Hata watumishi nao wakampiga makofi”.

   Hata baada ya watumishi waliofuata baada yake walikuwa wakiabudu dini hii ya KIYAHUDI kama PAULO. GALATIA 1:14Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kushika mapokeo ya baba zangu”.

  Lakini baada ya Paulo kuitwa na Bwana mambo yalibadilika wakaanza na kumshitaki. MATENDO 23:20-21Akasema Wayahudi wamepatana kukuomba umlete Paulo chini kesho, ukamweke mbele ya baraza, kana kwamba wataka kupata habari zake kwa usahihi zaidi. Basi wewe usikubali; kwa maana watu zaidi ya arobaini wanamwotea, wamefunga kwa kiapo wasile wala wasinywe hata watakapo mwua; nao sasa wako tayari, wakiitazamia ahadi kwako”.

   Ndipo Paulo anasema sijipendezi kwa wanadamu katika GALATIA 1:10Maana, sasa je! Ni wanadamu ninaowashawishi, au Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo”. 

    Ndipo Paulo anatuambia kutoka kwenye dini kuna faida kubwa GALATIA 1:15-16Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake, alipoona vema kumdhihirisha mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu;” hapa Mungu hakutaka Paulo abakie katika dini bali afundishe mapenzi yake kwa watu waliopo katika dini.

    Swali: ndani ya dini kuna nini ambacho hakimpendezi Mungu, na nje ya dini kuna nini ambacho ndicho sisi tunatakiwa tukiendee? Je! watakatifu wa zamani walikuwa na dini? MATENDO 11:26 Hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia, ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia”. Hiki ndicho kitu ambacho kinahitajika kwa sasa katika dini na madhehebu pasipo kujali huyu anaabudu siku gani au huyu anabatizwa kwa ubatizo gani au anatumia utaratibu gani au mfumo gani katika kuwasilisha haja zake mbele za Mungu. Kwasababu haijalishi unatumia utaratibu gani au mfumo gani katika kupeleka haja yako mbele za Mungu lakini haja zote humfikia Mungu mmoja tu.

     Lakini swali bado linabaki kuwa DINI ILIYO SAFI NI IPI? YAKOBO 1:27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo na mawaa”. Kinachotakiwa ndicho hicho vikiambatana na kuwa na neno la Kristo na kulitii.

    Wito wa Mungu kwetu sote ni kutuita sote twende kwake na si kutuita kwa majina ya dini au dhehebu maana yake haijalishi tumeshikilia dini au dhehebu kwa namna gani lakini Mungu anatuita kwa mwito mmoja na sote makao yetu ni pamoja tu. MATHAYO 11:28Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha”. Na pia katika YOHANA 10:10 anasema “Mwivi haji ili aibe na kuchinja na kuharibu, mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele”. Maana yake tunatakiwa kukimbilia kwa Yesu na sio kuukimbilia Dini na hapo ndipo wanadamu wengi tuliporudi nyuma kiimani kwa sababu ya kushikilia dini na kusahau kuwa katika dini kuna UTARATIBU au KANUNI na kumbe kusudi la Mungu sio utaratibu au kanuni za dini bali anachotaka Mungu ni kushika KUSUDI lake alilolileta kwa mwanadamu kupitia mwanae Yesu Kristo, soma YOHANA 10:27Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata”. 


     Na hapo ndipo ambapo wanadamu wengi tunafika kipindi tunaishi kwa utabiri wa nabii Isaya katika MATHAYO 15:7-9Enyi wanafiki ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, Wakifundisha Mafundisho yaliyo ya wanadamu”. Maana yake hicho ndicho kilichopo katika dini imefika wakati tunafundishana utaratibu na kanuni ambazo wanadamu wameziweka na sio ule utaratibu wa Mungu. Hivyo ndugu yangu tambua ya kuwa katika dini yamejaa maagizo ya wanadamu.

    Swali: je! ni vibaya kuwa na dini? La hasha! Dini zinatusaidia kupata mafundisho kutoka kwa waalimu, wachungaji, wainjilisti n.k yaani tunaweza kusema dini ni chanzo cha mwanadamu kujua karama yake na kuitumia/kuitumikia kwa kumzalia Mungu matunda.

   Biblia inasema katika HOSEA 4:6Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi, kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako; mimi nami nitawasahau watoto wako”.

MUNGU Awabariki na azidi kuibariki kazi yake idumu milele hata ukamilifu wa Dahari.

Karibu kwa maoni na maswali.


Comments

Popular posts from this blog

NGUVU ILIYOPO KATIKA NENO LA MUNGU

KIJANA NA USAFI WA MAISHA YA KIKRISTO

WAJIBU WA KIONGOZI {P2}